MALI TUTASHINDA AFCON – LASSINE SINAYOKO

Baada ya kuchangia pakubwa katika ushindi wa 2-1 wa Mali dhidi ya Burkina Faso katika mchuano wa hatua ya 16 bora, Lassine Sinayoko anasema bado kuna kazi kubwa ya kufanya huku timu yake ikipania kutwaa taji lao la kwanza la bara tangu waanze kushiriki mara ya kwanza mwaka 1972.

Licha ya kufika fainali mara tano, The eagles ni miongoni mwa nchi kubwa za Afrika ambazo bado hazijaweza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Mshambulizi huyo anayeichezea Ufaransa amepongeza uimara wa timu yake dhidi ya majirani zao, lakini akaonya kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanywa kwani mechi zinazofuata zitakuwa ngumu zaidi.

The Eagles ya Mali watamenyana na wenyeji Cote d’Ivoire katika robo-fainali mjini Bouake siku ya Jumamosi katika kile kinachoahidi kuwa mechi nyingine ya muondoano ya kishindo nchini Cote d’Ivoire

Kwa sasa mashindano ya Afcon yamesimama zinazosubiriwa ni mechi za robo fainali ambapo timu nane zitakuwa zinachuana kupiga mechi zao wanapoendelea kupigania ubingwa mwaka huu kuanzia tarehe mbili mwezi February unao anza kesho.