Klabu ya Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge imelazimishwa sare tasa na klabu ya Liverpool baada ya kuondoka kwa mkufunzi wao Graham Potter aliyefutwa kazi kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya.
Matokeo hayo sasa Chelsea kusalia katika nafasi ya 11 kwenye ligi wakati Liverpool ya mkufunzi Jergen Klopp ikishuka hadi nafasi ya nane.
Matokeo mengine ni kwamba Brighton walisajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth katika uwanja wa ugenini Vitality stadium huku Leeds United ikiitandika Nottingham Forest kichapo cha mabao 2-1 na hatimaye Aston Villa katika uwanja wa ugenini huko King Power wameitandika Leicester city kichapo cha mabao 2-1.

