SIOGOPI KUFUTWA – KLOPP

Mkufunzi wa Liverpool Jergen Klopp anasema hana shaka na kufutwa na klabu hiyo akisema kwamba wamiliki wa Liverpool wanafahamu vyema hali halisi ya klabu ya Liverpool kwa sasa.

Ameyasema hayo baada ya kupiga sare tasa dhidi ya Chelsea kwenye mechi ya ligi kuu uingereza iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Klopp amesema ingekuwa ndio mwanzo anajiunga na Liverpool na kuandikisha matokeo mabaya angekuwa ashafutwa lakini kwa sasa anaamini kwamba heshima yake kwa klabu hiyo inaezekana kuwa inamkingia kibarua chake kuota nyasi.

Mkufunzi huyo mjerumani amekaa Liverpool kwa kipindi cha miaka saba na ameishindia klabu hiyo mataji kadhaa makubwa yakiwemo Kombe la klabu bingwa ulaya, Uefa Super Cup, Kombe la ligi ya primia baada ya ukavu wa miaka 30 kwa klabu hiyo pamoja na taji la FA na Fifa Club World Cup.