TUTATETEA UBINGWA – MATANO

Mkufunzi wa klabu ya wanamvinyo Tusker fc  Robert Matano amesema vijana wake wako tayari kutetea ubingwa wao katika ligi ya fkf msimu huu.

Hii ni baada ya jana kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards katika uwanja wa nyayo.

Alama hizo tatu za jana zinawafanya kupunguza pengo lao na vinara wa ligi Gor Mahia kwa utofauti wa alama nne ikizingatiwa kwamba Tusker bado wanasalia kuwa na mechi moja kiporo.

Wakati hayo yakijiri, mkufunzi wa Gor Mahia Johnathan McKINSTRY amelalamikia maamuzi mabaya ya refa wa katikati ya uwanja yaliyoponza klabu yake katika mechi ya jana katika ligi kuu.

Kogalo jana walilazimishwa sare tasa dhidi ya batoto ba mungu sofapaka katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.