CHANZO CHA SS ASSAD KUKOSA MECHI ZA WIKENDI

Klabu ya SS Assad ilikosa kucheza mechi yake ya wikendi kutoka na kutopatikana kwa kadi za wachezaji kipindi cha mechi wakati wa ukaguzi na komishena wa mechi hiyo

Kulingana na taarifa kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo ya kaunti ya Kwale inashiriki ligi ya kitaifa ya Super League ni kuwa wapinzani wao Muhoroni walisusia mechi hiyo baada ya SS Assad kukosa kutimiza vipengee vyote vya kuheshimu ratiba kwa mujibu wa sheria za Fkf

Taarifa hiyo inasema kwamba kadi za wachezaji zimezuiliwa na aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo Phelix Ogutu.

Hata hivyo Assad wanasema walikuwa wamewasilisha lalama zao kwa ofisi za Fkf mapema wiki jana kuhusu utata wa kadi hizo.

Kwa sasa mechi hiyo ambayo haikuchezwa inasubiri maamuzi ya Fkf kuhusu mwafaka wake.