Serikali ya kaunti ya Kilifi inaendeleza ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni tano za maji, katika eneo la Mtepeni na lingine lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 2.5 kule Rabai.
Kulingana na gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro, hatua hiyo ni njia mojawapo ya kusaidia wananchi katika kukabiliana na suala la ukosefu wa maji ya mreji mashinani.
Akizungumza na wanahabari hapa kaunti ya Kilifi, Mung’aro amesema kuwa ujenzi wa matanki hayo, utagharimu takriban shilingi milioni 280 kwa jumla.
Aidha, amesema kuwa hatua hiyo pia itatoa suluhu la wananchi kukatiwa maji mara kwa mara, ili kutosheleza wananchi wa kaunti yote ya Kilifi na Maji, kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha katika kisima cha Baricho.

