KATIBU WA WIZARA YA AFYA MARY MUTHONI AWATA WANAWAKE KUFANYIWA UKAGUZI WA SARATANI YA KIZAZI.

Wito umetolewa kwa wanawake kujitokeza na kufanyiwa uchunguzi dhidi ya Saratani ya Kizazi.

Akitoa wito huo, katibu katika wizara ya afya nchini Mary Muthoni, amesema kuwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 15, wanapaswa kupewa chanjo ya HPV, iliyo na uwezo wa kuwakinga dhidi ya maradhi ya Saratani ya kizazi.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari, katibu Muthoni amesema kuwa idadi kubwa ya maradhi kwenye jamii, yanaweza kudhibitika iwapo yatatabuliwa mapema.

Muthoni aidha amesisitiza haja ya jamii kuchukuliwa kwa uzito suala la kuwalinda wasichana dhidi ya uongozi wa Saratani ya kizazi, kwa kufuata ushauri wa wizara ya afya nchini.