Meneja wa klabu ya Young Bulls kutoka Malindi kaunti ya Kilifi Hussein Captain Garga anasema klabu hiyo imepata pigo kubwa baada ya kushindwa kuheshimu ratiba ya wikendi hii dhidi ya Marafiki Fc pale klabu hiyo ilishindwa kusafiri hadi kaunti ya Nyeri
Kulingana na Garga klabu hiyo inapitia changamoto chungu nzima jambo ambalo linafanya timu hiyo kuwa katika hatari ya kushuka daraja iwapo mambo hayatabadilika
Garga akizungumza na Tama La Spoti kupitia njia ya simu Garga anasema sasa ipo haja suluhu la haraka kupatikana ili kuuokoa msimu huu ambao ndio wao mbovu katika historia ya timu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.
”Kwa sasa klabu inapitia changamoto chungu nzima, itabidi tujipange upya angalau sehemu ya pili ya msimu huu tuikwamue timu. Hii inatuhitaji sote kama washikadau” Alisema Garga
Kwa sasa klabu hiyo iko nafasi ya mwisho katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa

