Mtendaji Mkuu wa Bumbani Stars Rajab Zamani, Amekanusha madai kwamba waliikosa sajili ya Mchezaji Bora wa Dola Cup Feiswal Dzuya mwaka jana kwa Klabu ya NSL AS Assad, akidai kwamba aliyapa nafasi mazungumzo kati ya Pande Hizo Mbili.
Zamani ameongezea kwa Kusema ya kwamba wapo kwenye Harakati za kumnasa nyota Huyo, hii ni Baada ya Dzuya Kuachana Na Assad Novemba mwaka jana kufuatia Sintofahamu kati yake na mkufunzi phelix Ogutu, na Kurejea kwao Nyumbani eneo la Mjanaheri eneobunge la Magarini Kaunti ya Kilifi.
Asubuhi ya leo Bumbani Stars wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Riruta kaunti ya Nairobi, wakijinoa makali kwa ajili ya mechi yao ya Kesho Dhidi ya ZetechTitans.
Klabu hiyo inashiriki msimu wake wa kwanza katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa iliachana na mkufunzi wake wa zamani MWADUKA Bakari kabla ya kuanza ya kuanza msimu huu.

