UEFA KUFANYA MABADILIKO

Baada ya kuleta Mfumo mpya wa Kuzishirikisha timu thelathini na Sita kwenye Michuano ya UEFA, Hivi sasa Shirikisho la Soka la KLabu Bingwa Ulaya linapania kuleta marekebisho mengine ligini, likitaka kudondosha muda wa Nyongeza kuelekea kwenye Mechi za Mchujo.

Hii Ni Kumaanisha ya kwamba iwapo Mshindi hatapatikana baada ya Dakika Tisini za Mechi, basi Moja kwa Moja  wachezaji watalazimika kupiga Mikwaju ya Penalti ili kubaini Mshindi.

Iwapo marekebisho haya yatafanywa, Basi  ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itachkua Mkondo ule wa Kombe la FA.

UEFA msimu huu imechukua mkondo tofauti ikileta mabadiliko makubwa hasa hatua ya makundi wachanganuzi ulaya wakitaja kuwa mashindano hayo msimu huu yaliletwa kwa lengo ya kuyapanua.