Rais wa fkf hapa nchini Hussein Mohammed amewataka wachezaji walioteuliwa na mkufunzi Benni McCarthy kuipeperusha bendera ya Kenya vyema katika majukumu yao ya kitaifa watakapokuwa wanachuana na Gambia wiki hii kwenye mechi ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2026.
Hussein kupitia ukurasa wake rasmi wa facebook ametaja kuwa walifanya kikao cha himizo kwa wachezaji hao jana, kikao kilichohudhuriwa na naibu rais McDonald Mariga pamoja na viongozi wengine.
Harambee Stars wamesafiri leo kuelekea Gambia ambako watachuana na timu ya taifa hilo inayoongozwa na kocha wa zamani wa klabu ya Gor Mahia nchini, Johnnathn McKintry.
Mckinstry katika mahojiano ya hivi punde na vyombo vya habari anasema anatarajia ushindani mkubwa kutoka Kenya kwani chini ya uongozi mpya Kenya inatarajiwa kuleta mwamko mpya akitaja kuwa kocha Benni katika historia yake amekuwa kocha wa kupenda kushambulia akiwa Amazulu au hata Cape Town City.
Hili litakuwa jukumu la kwanza kwa Benni McCarthy kama kocha mkuu wa Harambee stars akichukua pale Fransic kimanzi kocha wa muda wa timu hiyo alipoachia.
Nahodha wa timu ya taifa ya Harambe Stars Michael Olunga ameelezea furaha yake kwa sapoti nzuri wanayopata kutoka kwa shirikihso la soka nchini akitaja kuwa wameweka mazingira mazuri ya wachezaji kuja Kenya kwa ajili ya kujiandaa kwa mechi za kimataifa.
