Juhudi za klabu ya AFC Leopards za kumaliza ukame wao wa Mataji zimegonga Mwamba, klabu hio Ikibanduliwa nje ya michuano ya FKF cup na kamati ya ligi ya mashindano ya FKF, hii ni baada ya mechi kati yao na Mara Sugar Kusitishwa mashabiki wa Ingwe walipozua Rapsha.
Rapsha Hio ilizuka kwenye dakika Za lala salama ya leopards walipopata penalati, lakini mwamuzi wa kati baada ya kushauriana na wa kando alibatilisha Uamuzi Huo, Kitu ambacho Kilichangia mashabaki wa Ingwe Kuingia Uwanjani, mechi hio iliyopigwa Siku ya Jumamosi Huko Kisumu Ikisimamishwa.
Matumaini ya Leopards kupata taji msimu huu sasa Yamesalia kwenye ligi Kuu hapa Nchini, lakini hawajakua wakiandikisha matokeo bora wakishikilia nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi, na alama thelathini na sita baada ya Mechi ishirini na tatu.

