RATIBA YA LIGI YA UKANDA WA PWANI YATOKA

Ratiba ya ligi ya kanda ya Pwani ya Zone B Inayojumuisha Kaunti za Kilifi, lamu na Tanariver, hatimaye imeweza kutoka  timu thelathini zilizogawanywa kwenye makundi mawili, zikijitosa kwenye Kinyang’anyiro hicho cha Kusaka nafasi kwenye divisheni ya pili.

Kundi A litazikutanisha Timu kumi na tano ikiwa ni pamoja na Washindi wa ligi ya Kaunti ya Kilifi msimu Uliopita Rocky, wapinzani wao wa jadi Chasimba United, Kisumu Ndogo United kutokea Mjini Malindi, Bahari na Dose Fc kutokea Mpeketoni, pamoja na Malindi Progressive walioshukishwa Daraja kwenye Divisheni ya Pili.

Kundi B linajumuisha Silver Bullets kutokea Vipingo ambao pia walishukishwa daraja, msato fc ya Msabaha, Uhuru Strikers ya Garsen, hindi boys ya Lamu pamoja na GFC Kutokea eneo la Gongoni, huku Raundi za Kwanza za Michuano Hii Ikitarajiwa kupigwa wikendi hii ya Tarehe ishirini na mbili.