BANDARI KUREJEA MBARAKI JUMAPILI

Klabu ya Bandari FC itaanza rasmi kutumia uwanja wa Mbaraki Sports Club Jumapili baada ya kuchezea viwanja Mombasa Sports Ground pamoja na uwanja wa Ukunda Show Ground kwa muda kipindi ambacho uwanja wao wa nyumbani ulikuwa unaundwa kupewa hadhi ya kimataifa.

Mechi ya kwanza kuchezwa katika uwanja huo ni dhidi ya Shabana FC mbandari wakiwa na lengo la kuandikisha matokeo mazuri katika dimba hilo.

Taarifa zasema kuwa takriban milioni 300 zilitumika kuuboresha uwanja huo, mamlaka ya bandari ikisadikika ndio uliokuwa inasimamia ukarabati huo.

Mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo kwa sasa wana njaa ya kuandikisha matokeo bora kwani mechi tano zilizopita klabu hiyo haijaandikisha ushindi hata mmoja.

Kwa sasa Bandari FC inasimama katika nafasi ya 7 ligini wakiwa na alama 22