Maafisa wanane wa serikali ya kaunti ya Tana River wametiwa nguvuni na maafisa wa tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC kwa madai ya kushiriki kwenye ufisadi wa shilingi milioni 9.
Akithibitisha hilo afisa wa mawasiliano katika tume hiyo Eric Ngumbi, amesema kuwa wanane hao ni kali ya washukiwa 14 ambao wanadaiwa kutoa zabuni kwa njia ya ulaghai kwa kampuni ambayo haikuwa imeafikia vigezo hitajika kisheria ili kutekeleza zabuni yeyote.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari hapa mjini Malindi, Ngumbi amesema kuwa wanane hao wametafikishwa mahakamani hii leo na kufunguliwa mashtaka ya ufisadi dhidi yao.
Msemaji huyo wa EACC, Amedokeza kuwa Tume hiyo inawasaka washukiwa wengine 6 wanaoaminika kutoroka.

