BODABODA KUSHIRIKI LIGI YA FKF

Muungano wa Bodaboda katikaeneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wikendi hii utakuwa unaadhimisha mwaka mmoja wa kuundwa kwa kikosi cha soka na muungano huo maarufu kama MAUMORI Sports Clubs.

Kulingana na mwenyekiti wa Bodaboda hao Nzai Randu ni kuwa wamepanga mechi ya kirafiki itakayochezwa hiyo kesho katika uwanja wa Alaskan dhidi ya timu ya muungano wa bodaboda kutoka Rabai Kisurutini.

Randu akizungumza na Tama la SPoti anasema lengo kubwa la mechi hiyo mbali na kuadhimisha mwaka ni pamoja na kuwaleta pamoja washikadau mbalimbali kwa lengo la kutoa hamasa za wafanyibiasha hao wa bodaboda miongoni mwa masuala mengine.

Randu amethibitisha kuwa timu hiyo ya Bodaboda wanalenga kuisajili katika ligi ya FKF katika tawi la eneo bunge la Malindi kuanzia msimu ujao ili kuzidi kulea vipaji vya soka katika jamii hususan vijana ambao pia wanafanya biashara hiyo.