AKIDA AACHANA NA AC PAOK UGIRIKI

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Moving the Goal post kutoka kaunti ya Kilifi Essie Akida sasa ni rasmi ameachana na klabu yake ya AC Paok Ugiriki baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa takriban miaka mitatu.

Akida amethibitisha hilo kupitia kurasa zake ya mitandao ya kijamii na kuonyesha mapenzi na klabu hiyo licha ya kusema kwamba kwa sasa anaondoka.

Akida ambaye bado hajatangaza anahamia klabu gani kuelekea msimu ujao aliwahi kushinda tuzo la mshambuliaji bora kwenye msimu wake wa kwanza kwenye mashindano ya Uefa ya kinadada.

Ameushukuru uongozi wa klabu hiyo hasa wakufunzi, wachezaji wenza pamoja na mashabiki kwa jumla.