ABABU AMSHUKURU RUTO BAADA YA KUFUTWA

Aliyekuwa waziri wa michezo hapa nchini Kenya Ababu Namwamba ameushukuru uongozi wa rais William Samoei Ruto kwa kumpa ya kuhudumia taifa hili katika sekta ya michezo. Ametoa shukrani hizo baada ya kufutwa jana wakati ambapo rais alitangaza kuwaachisha kazi mawaziri wote isipokuwa waziri mkuu na wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi.

Ababu katika ujumbe wake kwenye kurasa zake za kijamii anasema ni heshima kubwa kulifanyia kazi taifa hili nikinukuu taarifa yake kwenye ukurasa wa facebook anasema

‘’ Ni heshima, fursa na maalum kutumikia taifa langu, zaidi katika Baraza la Mawaziri, chombo cha juu zaidi cha kutengeneza sera nchini. Ninamshukuru Mheshimiwa Rais William Samoei Ruto kwa imani na imani iliyosababbisha kuteuliwa kwangu kuhudumu katika Baraza la Mawaziri kwa mara ya pili katika maisha yangu ya utumishi wa umma. Mungu ibariki Kenya na amjalie Rais neema na hekima kuelekeza nchi yetu katika njia salama.’’ Alisema Ababu

Ababu aliwahi kuwa waziri wa michezo kwa muda mfupi katika kipindi cha rais wa zamani Hayati  mwai Kibaki kabla ya kuteuliwa tena na rais wa sasa William Ruto mwaka 2022