Mabingwa mara 12 wa ligi kuu nchini Kenya AFC Leopards wamesajili ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya klabu ya Talanta FC katika mechi iliyochezwa dimbani Nyayo mtanangwe uliochezwa mchana wa leo.
‘Hatrik’ ya fowadi Victor Omune raia wa DRC Congo pamoja na mabao mawili ya Cliff Nyakeya ndiyo yaliyotosha kuwapa ushindi vijana hao wa mkufunzi Patrick Aussems.
Matokeo hayo sasa yanaifanya AFC Leopards kupanda hadi nafasi ya tano wakiwa na alama 25 huku Talanta FC ikishuka hadi nafasi ya 14 na alama 12.
Katika dimba la Kasarani Posta Rangers wamepiga sare ya baao 1-1 dhidi ya klabu ya Wazito FC.

