Mkufunzi mkuu wa klabu ya Sango Sportiff timu ya pekee inayowakilisha kaunti ya Tana River katika ligi ya daraja la pili kitaifa mwite Righo Jillo anasema ako na matumaini makubwa ya kusajili ushindi wikendi ijayo ambapo vijana wake watasafiri kwenda Lamu kuvaana na klabu ya Deep Sea.
Mkufunzi huyo amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kusimama kidete nayo na licha ya kuwa na mwanzo mbovu msimu huu, Jillo akikiri kuwa wamekabiliwa na changamoto mbali anaimani kubwa kwamba kila kitu kitakuwa shwari na kuanza kusajili ushindi.
Huu ndio msimu wa kwanza kwa Sango Sportiff kucheza ligi ya daraja la pili baada ya kuwa na matokeo mazuri katika ligi ya mkoa msimu uliopita.

