Waziri wa michezo Ababu Namwamba hii leo amebatilisha uteuzi wa kamati ya talanta hela aliyoichagua mwezi February kusaidia masuala ya michezo pamoja na talanta hapa nchini Kenya.
Awali kamati hiyo iliyofaa kuhudumu kwa miezi mitatu katika kusaidia makuzi ya talanta pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kwamba wachezaji wa Kenya hawapitii changamoto zaidi hasa mashinani.
Waziri ababu amelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na mahakama kuharamisha utekelezwaji wa kamati hiyo.
Mradi wa Talanta hela ulifaa kuzinduliwa rasmi hii leo na rais William Samoei Ruto.

