ALEX MWALIMU KUENDELEA KUKOSA MECHI ZA YOUNG BULLS

Klabu ya Young Bulls itazidi kumkosa mshambulizi wake nguli Alex Mwalimu mzawa wa Matsangoni kaunti ya Kilifi kutokana na majeraha.

Alex aliumia katika mechi ya Mudzini Derby dhidi ya Malindi Progressive ambapo walishinda kwa bao 1-0 mwezi mei.

Kwa sasa Young Bulls itakuwa bila mshambuliaji huyo ambaye amewasaidia sana msimu huu katika kusajili matokeo mazuri.

Katika mechi za hivi punde Youngs Bulls bila Alex Mwalimu ilipoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Kibra Soccer jijini Nairobi na kupiga sare baadae dhidi ya Olympics Pirates.

Wikendi ijayo Young Bulls watakuwa wanaikaribisha Administration Police katika uwanja wa shule ya Upili ya wavulana ya Malindi kaunti ya Kilifi.