Shirikisho la Soka FKF, Limeahirisha Kwa Muda Mafunzo Yote ya Ukocha ya CAF Daraja ya D kote Nchini, hadi katikati ya mwezi wa Mei mwaka Huu.
Katika Taarifa Iliyoelekezwa Kwa wenyeviti wa Matawi ya FKF, Mkurugenzi wa Maendeleo wa FKF Francis Kimanzi ameelezea Kuwa Hatua Hiyo,
Inalenga Kuoanisha Mafunzo hayo na Viwango vipya vinavyoendelea Kubadilika, vilivyowekwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF.
Kozi ya CAF Daraja Ya D ni uthibitisho wa ngazi ya kwanza unaolenga makocha wanaotamani kuwa na ufanisi, na inazingatia maendeleo ya soka la msingi.
Programu hii ya siku kumi inajumuisha kanuni za msingi za ukocha, ikiwa ni pamoja na tathmini ya wachezaji, kupanga na kufanya mazoezi, na kutekeleza mikakati ya kimatiki.
Washiriki wanaomaliza kozi hii wanatakiwa kufanya mazoezi ya ukocha kwa angalau mwaka mmoja kabla ya kuendelea na leseni ya CAF Daraja la C.

