GACHAGWA AONGOZA MRENGO WA UPINZANI KATIKA KUKASHIFU SERIKALI YA RAIS WILLIAM RUTO.

Viongozi wa upanzani nchini wakiongozwa na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, amemsuta rais William Ruto kwa kuchangia matatizo mbali mbali ya wakenya.

Kulingana na viongozi hao, tayari wameanza mikakati ya kuhakikisha kuwa wanaungana pamoja na kumuondoa rais William Ruto mamlakani, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Gachagwa amesema amewataka wakenya kutokubali kuhadaiwa na serikali ya Kenya kwanza kwa madai kuwa imeshindwa kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumza katika eneo la Mlolongo kule kaunti ya Machakos, Gachagwa amemuonya kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka dhidi ya kuungana tena na Raila Odinga katika masuala ya kisiasa.

Vile vile amewataka vijana wa kizazi cha Gen Z hapa nchini kenya  kutafuta vitambulisho vya kitaifa na kuhakikisha kuwa wanasajiliwa kuwa wapiga kura kwani ni mojawapo ya harakati za kumuondoa rais William Ruto mamlakani.

Kwa upande wake Kalonzo Musyoka pamoja na Eugene Wamalwa ameunga mkono kauli hiyo huku wakiahidi kutetea wanasiasa wanaotishiwa na serikali ya kitaifa kutokana na hatua yao kukosoa uongozi wa serikali kuu.