KILIFI YAPANGWA KUNDI D KYISA

Timu ya Kilifi County Imepangwa tena Kwenye Kundi D Pamoja na Kaunti ya Nyeri na Nakuru,  kwenye Makala ya Kumi ya   mashindano ya KYISA yatakayoanza hii leo, kaunti hizo zikipangwa tena kwenye Makala yaliyopita yalioandaliwa katika Kaunti Ya Kilifi.

Timu hiyo ya soka ya wanaume itaanza harakati zake za kusaka Ubingwa Kwenye Mashindano Hayo, Dhidi ya Kaunti Nakuru Saa tatu asubuhi hapo kesho katika Uwanja wa shule ya Upili ya Wikoteng, kabla Ya kurudi Dimbani saa nane mchana kucheza Mechi ya Mwisho ya Makundi Dhidi ya kaunti ya Nyeri.

Mechi za robo Fainali Zitapigwa siku ya Alhamisi Tarehe Kumi na saba, zile za Nusu Fainali na za Mchujo zichezwe Siku ya Ijumaa tarehe kumi na Nane, Huku Kilele cha makala hayo ya Kumi ikiwa tarehe Kumi na tisa Siku ya Jumamosi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *