KWALE NA TAITA TAVETA ZASUSIA KYISA

Maswali yanazidi kuibuka kuhusu ushiriki wa kaunti za Kwale na Taita Taveta kwenye mashindano ya KYISA ambayo hufanyika kila mwaka.

Mwaka huu mashindano hayo yanafanyika katika kaunti ya Homa Bay na kwa mara nyingine tena kaunti hizo bado hazijawasilisha timu kwa ajili ya mashindano hayo ya kitaifa.

Kaunti za Lamu, Tana River na Kilifi ndio kaunti za hivi punde ambazo zimetuma timu zao katika mashindao hayo ambayo ni makala la 10.

Ikumbukwe kuwa makala ya mwaka jana, kaunti za Taita Taveta na Kwale hazikushiriki licha ya kuwa mashindano hayo yalikuwa yanafanyika katika kaunti ya Kilifi.

Baadhi ya wadau wa soka mitandaoni wakiyaapuzilia mbali yamshindano hayo wakisema hayajakuwa na manufaa yoyote kwa mchezaji mashinani wengine wakitaja ukosefu wa raslimali za kushiriki mashindano kama hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *