SERIKALI YA KITAIFA YAPANIA KUNUNUA MAGARI ELFU TANO YA MAAFISA WA POLISI KITAIFA.

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, amesema kuwa serikali inapania kununua magari elfu tano, yatakayo kabidhiwa maafisa wa polisi.

Kulingana na Murkomen, idadi kubwa ya majukumu ya maafisa wa polisi katika taifa hili, yamekosa kufanikishwa kutokana na ukosefu wa usafiri.

Akizungumza hapa kaunti ya Kilifi, waziri huyo amesema pia kuna haja ya matatizo ya maafisa wa utawala kuangaziwa kiukamilifu, katika maeneo yote ya taifa hili.

Kwa upande wake mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi Amina Mnyazi, amesema kuwa kituo cha polisi hapa mjini Malindi, ni mojawapo ya maeneo ambayo yamekosa kuendeleza majukumu yake kwa wananchi, kutokana na ukosefu wa magari ya maafisa wa polisi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *