Wizara ya afya nchini, imetoa hakikisho la kukabiliana na mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu katika kaunti 11 za taifa hili.
Katibu katika wizara ya afya nchini Daktari Mary Muthoni, amesema kuwa kufikia sasa visa 97 vya watu walioaga dunia, baada ya kuugua maradhi hayo vimeripotiwa kitaifa.
Katibu huyo amesema kuwa pia wanaendeleza juhudi za kuwasaka baadhi ya wale waliotangamana na waathiriwa hao wa maradhi ya kipindupindu.
Aidha, amesema kuwa tayari baadhi ya wagonjwa wamewekwa katika karaniti, ili kuwazuia dhidi ya kusabaza maradhi hayo zaidi.