Waziri wa madini na uchumi wa bahari na maziwa nchini Ali Hassan Joho amenyooshea kidole cha lawama mashirika ya kijamii, kwa kutatiza shughuli za uchimbaji madini eneo bunge la Ganze hapa kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Joho, mashirika ya kijamii pia yamechangia kusimamishwa kwa shughuli za utekelezwaji wa miradi ya maendeleo, hasa katika wizara yake.
Akizungumza katika mahojiano na runinga moja kitaifa, joho amesema kuwa hatua hiyo, imetatiza utendakazi wa wizara yake, licha ya wananchi kukubali kufanyiwa miradi hiyo kwenye jamii.
Aidha, Joho ametoa wito kwa jamii kukumbatia masuala ya uchimbaji wa madini na kuhakikisha kuwa wanafanya vikao vya kupambanua masuala mbali mbali, kuhusiana na shughuli za uchimbaji madini husika katika maeneo yao.