Mbunge wa Githunguri kaunti ya Kiambu, Gathoni Wamuchomba, amedai kwamba maisha yake yako hatarini baada ya serikali kuu kumpokonya walinzi wake.
Wamuchomba ambaye pia ni mwandani wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema analengwa kutokana na msimamo wake wa kisiasa.
Akizungumza baada ya kuandikisha taarifa katika afisi za kitengo cha DCI, Wamuchomba amesema kuwa rais William Ruto, anatumia maafisa wa serikali kuwapiga vita wapinzani wake kitaifa.
Wamuchomba vile vile amekashifu hatua ya kiongozi wa taifa kutolaani vitendo vya baadhi ya wanasiasa, kuvamiwa na magenge ya vijana wakati wanapo hudhuria ibada.

