GARGA AFICHUA KILICHOWAHAMISHA ALASKAN

Meneja wa klabu ya Young Bulls inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa Hussein Capt Garga anasema matumaini bado yapo klabu hiyo itasalia katika ligi hiyo licha ya wamzno mbovu msimu huu iwapo itashikwa mkono.

Amesema hayo baada ya wikendi hii klabu hiyo kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zetech Titans katika uwanja wa Malindi High.

Amesema changamoto kubwa waliyonayo Young BULLS ni ukata wa kifedha na iwapo wachezaji watashikwa mkono na kupata motisha huenda wakafanya maajamu katika mechi saba zilizosalia.

Garga vilevile ametoa sababu ya kilichowafanya kuugura uwanja wa Malindi High akitaja kuwa uchache wa mapato pamoja na vilabu vingi kuutumia uwanja huo kuliwafanya kuondoka na kurejea uwanja wao wa Malindi High ambao ni karibu na kambini.