LUKAKU AFIKISHA MABAO 400

Mshambuliaji wa Klabu ya Napoli na Timu ya taifa Ya Ubelgiji Romelu Lukaku , hapo jana usiku alitinga  Goli Lake la Kihistoria kwenye Ushidi wa Napoli Dhidi Ya Ac Milan, akifikisha Ujumla Wa Magoli mia nne  kwa Klabu yake Na Timu ya Taifa.

Kwenye Taaluma yake Ya Miaka Kumi na Sita Lukaku ameziwakilisha Timu nane Tofauti, Nne kwenye Kwenye Ligi kuu Ya  Uingereza ambazo Ni pamoja Na Chelsea, West Brom, Everton na Manchester United, Tatu kwenye Sereie A akizichezea klabu za InterMilan, Roma na Napoli, na Moja kwenye Timu yake ya Nyumbani ya Anderlecht Nchini Ubelgiji.

Mshambuliaji Huyo amekua na wakati Mzuri na klabu za Everton na InterMillan, Akifunga magoli  themanini  na Saba na Sabini Na nane Mtawalia, akiwa na Kibarua Kizito Stamford Bridge  alipoliona Lango mara Kumi na Tano Baada Ya Mechi Hamsini Na Tisa, akifunga magoli mia moja Ishirini na Moja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, kumi na Nane kwenye Klabu Bingwa Ulaya na Ishirini na Saba  kwenye Ligi Ya Europa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *