BRUNO FERNANDES HAENDI POPOTE – AMORIM

Mkufunzi wa Klabu ya Manchester United Ruben Amorim, ameyakanusha Madai ya Kuwa Huenda Nahodha Wa Kikosi Chake Bruno Fernandes, akajiunga na Miamba wa Uhispania Real Madrid  kwenye Majira Yajayo ya Joto.

Fernandes Ambaye amekuwa Kwenye Ubora wake Msimu Huu, amecheka Na wavu mara Saba kwenye Mechi saba Zilizopita, Kiungo Huyo Wa Kireno akifunga magoli Kumi na sita msimu Huu na Kupeana Asisti kumi na Tano.

Baada ya Mapumziko ya Kitaifa  Ligi Kuu ya Uingereza Imerejea Rasmi Hii leo, United wakiekeana Miadi na Nottingham Forest saa Nne Usiku Hii leo. Klabu ya Manchester City, wameonyesha azma ya Kutaka Kumsajili beki wa Arsenal na Timu ya Taifa Ya Ufaransa Willliam Saliba, kwenye Majira yajayo ya joto huku Saliba Pia akiwa Kwenye Rada za Real Madrid.