GREENWOOD AACHANA NA UINGEREZA

Mshambuliaji wa Zamani wa Manchester United ambaye Hivi sasa Anakipiga na Klabu ya Marseiile ya Ufaransa Mason Greenwood, hapo Jana ALIAMUA Kuachana na Ndoto ya kulichezea Tena taifa La Uingereza, Katibu Mkuu wa FA akithibitisha Kuwa Nyota huyi ameomba Kuichezea Jamaica.

Greenwood ameshinda Mechi Moja Pekee na the Three Lions, kabla Ya Kudondoshwa Nje ya Kikosi Hicho akikamatwa na Tuhuma za Ubakaji janauri mwaka wa Elfu mbili ishirini na Mbili, Mashtaka hayo Yakifutwa Februari mwaka wa Elfu Mbili ISHIRINI NA TATU.

Kufikia Sasa, Green wood amefunga Magoli kumi na matano baada ya mechi Ishirini na Nne na Upande Huo wa Ufaransa  msimu Huu.