Neymar ameweza Kapata mwaliko kwenye Timu ya Taifa Ya Brazil, baada ya Kukaa Nje kwa Takriban mwaka mmoja na Nusu, akiuguza Jeraha kwenye mechi dhidi ya Uruguay oktoba mwaka Juzi.
Baada ya Jeraha Hilo Mshambuliaji huyo mwenye umri wa Miaka Thelathini na mitatu alijitahidi vilivyo Kurudisha Fomu Yake, akiwa Na Matumaini ya kuwakilisha Samba Boys Kwenye Kombe la Dunia La mwaka Wa Elfu mbili Ishirini na Sita, ambapo taifa la Canada, mexico na Marekani watakua wenyeji.
Neymar aliachana na upande Wa Saudi Arabia Al Hilal mapema mwaka Huu, akicheza mechi saba pekee akizongwa na Majeraha , kabla Ya Kurudi kwenye Timu yake ya Utotoni Santos ambapo amefunga magoli matatu na Kupeana Asisti tatu baada ya Mechi Saba.

