MECHI YA BUMBANI STARS YAAHIRISHWA

Mechi kati ya Bumbani stars na Kenya Navy ambayo awali Ilipangwa kuchezwa siku ya Jumapili terehe tisa Machi, imeahirishwa hadi tarehe kumi na mbili siku ya Jumatano wiki ijayo, Uamuzi huu ukiafikiwa na Uongozi wa Ligi baada ya Wachezaji wa Bumbani stars, kupata Majeraha kutokana na Vurugu Zilizotokea wakati wa mechi ya fkf kwale cup Dhidi ya Rainbow FC.

Kutokana na hali hiyo, Bumbani stars wamepewa muda wa ziada  ili kurejesha fomu yao, kwani baadhi ya wachezaji ikiwemo wakufunzi wao, waliweza Kuuguza majeraha wakati wa Vurugu Hio.

Kulingana na Taarifa Rasmi Iliyochapishwa kupitia mitandao yao ya Kijamii, upande huo wenye maskani yake kwale county  umesema kwamba tayari Kuna Hatua zinazoendelewa Kuchukuliwa, ili Kuhakikisha kuwa wote waliohusika watachukuliwa Sheria Ipasavyo.