Rais William Ruto amewahakikishia wakenya kuwa serikali yake itatekeleza haki na usawa, katika kutoa huduma zake kwa wananchi pasi na ubaguzi.
Rais ambaye amezungumza katika eneo la Eastleigh kule kaunti ya Nairobi mda mfupi uliopita, amesema kuwa sharti kila mkenya apewe huduma za serikali pasi na kuzingatia kabila lake ama tabaka.
Kiongozi huyo amesema kuwa kila mkenya, anahaki ya kupewa kitambulisho pasi na kupigwa msasa ili kuthibitisha uraia wake.
Aidha, Mtaa wa Eastleigh ni mojawapo ya mitaa iliyo na idadi kubwa ya wakenya wenye asili ya taifa la Somalia.

