WAKAAZI WA KAUNTI YA MOMBASA WATAKIWA KUUNGA MKONO MUUNGANO WA RAIS WILLIAM RUTO NA RAILA ODINGA.

Waziri wa madini na uchumi wa rasilimali za bahari na maziwa nchini Ali Hassan Joho, amewataka wakaazi wa eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa, kuunga mkono hatua ya Raila Odinga kuungana na Rais William Ruto.

Kulingana na Joho, muungano huo, unatarajiwa kuleta umoja na uwiiano kati ya viongozi wa mirengo mbali mbali ya kisiasa, sawa na kuchangia kushuhudiwa kwa umoja kati ya wakenya.

Akihutubia wananchi katika eneo hilo, Joho amesema kuwa kwa sasa, wananchi wa maeneo mbali mbali katika taifa hili, watanufaika na miradi ya maendeleo pasi na ubaguzi wa kisiasa.

Kwa upande wake gavana wa kaunti hiyo ya Mombasa, Abdulswamaad Shariff Nassir ameweka wazi kuwa chama cha ODM, hakija tupiliwa mbali ila ni viongozi tuu ambao wameungana, kwa malengo ya kuhakikisha kuwa mwananchi ananufaika, Kauli iliyo meungwa mkono na seneta wa kaunti hiyo Mohamed Faki.