Mchezaji wa Zamani wa Afrika Kusini na Kimataifa Benni McCarthy, ametambulishwa Rasmi kama Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Soka ya Wanaume hapa Nchini Harambee Stars, katika sherehe ya Kipekee Iliyoandaliwa Na Shirikisho la Soka FKF Hapo Jana.
McCarthy mwenye Umri wa Miaka Arubaini na Saba Alitia Saini mkataba wa Miaka miwili, na Majukumu yake ya kwanza yatakua kwenye mechi Za Kufuzu kwa kombe la Dunia la Mwaka Ujao mwezi Huu, stars watakapomenyana na Gambia na Gabon, na Kisha baadae kwenye Michezo Ya ndani ya Chan mwezi wa Agosti.
Mshindi Huyo wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya amekuja na Benchi lake la Ufundi Lililosheheni, ambalo Linajumuisha Vassili Manousakis kama Kocha Msaidizi, Joseph Moeneeb kama Kocha wa Makipa na Pilela Maposa kama Mchambuzi wa Utendaji.

