MHASIBU MKUU WA SERIKALI ATILIA SHAKA MITANDAO YA BIMA YA SHA.

Bunge la kitaifa pamoja na lile la seneti, limetakiwa kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wanaotoa kandarasi za mitandao, katika utekelezwaji wa bima mpya ya SHA.
Mhasibu mkuu wa serikali Nancy Gathungu, ameelezea wasiwasi wa wakenya kupoteza mabilioni ya fedha, katika bima hiyo iwapo bunge hilo halitaingilia kati suala hilo.
Gathungu ambaye alifika mbele ya kamati ya fedha kwenye bunge la kitaifa, amewataka viongozi hao kutilia maanani ripoti yake, kuhusiana na uozo ulioko kwenye bima mpya ya SHA.