MADAKTARI WATISHIA KUANDAMANA ILI KUPINGA UTUMIZI WA SHA.

Muungano wa madaktari nchini KMPUD, umetoa makataa ya wiki mbili kwa serikali ya kitaifa, kutatua changamoto zinazo kabili mpango wa huduma za matibabu kwa maafisa wa serikali, kupitia bima ya afya ya SHA.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano huo daktari Davji Atella, amesema kuwa iwapo serikali haita tekeleza hilo, watachukua hatua ya kuandamana na kisha baadae kufanya mgomo, hadi pale serikali itakapo sikiza matakwa yao.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari kaunti ya Nairobi, Atella ameilaumu serikali ya kitaifa, kwa kuchangia katika hali ngumu za maafisa hao na wakenya kwa jumla kutafuta huduma za matibabu kwa maafisa hao, licha yao kuchangia kwenye hazina ya bima mpya ya SHA.

Aidha, amesema kuwa sharti serikali irejeshe fedha ambazo, imekuwa ikitoza maafisa wa umma kila mwezi, kwani hawanufaiki na mpango huo.