Klabu ya Nottingham Forest imefuzu kwenye hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Emirates FA Cup, wakiwabandua Ipswich kwenye Kinyang’anyiro Hicho kupitia mikwaju ya Penalty, baada ya Kutoka Sare kwenye Muda wa Kawaida.
Kufuatia Ushindi Huo Nottinghama Forest sasa wataekeana Miadi Na Brighton, Manchester City dhidi Bournmouth, Preston Dhidi ya Aston Villa, Huku Fulham waliowabandua Mabingwa watetezi Manchester United wakivaana na Crystal Palace, Mechi Hizi Zikiratibiwa Kupigwa Tarehe Ishirini na Tisa mwezi Huu.
Juventus Hali kadhalika waliendeleza Fomu yao Bora, wakienda Mechi tano Bila Kupigwa walipopata Ushindi wa Magoli mawili sufuri Dhidi ya Verona.

