ALFRED CHOLE AELEZA SABABU ZA KUCHANA NA MOFA

Alfred Chole Mkufunzi wa MOFA Klabu inayamilikiwa na Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga, ameeleza sababu zake za Kujihuzulu, kufuatia Kipigo cha Magoli mawili sufuri na Mombasa United siku ya Jumatatu huko Serani.

Chole ambaye alichukua Hatamu hio mwanzoni mwa msimu Huu alipoachana na APS Bomet, ameelezea kuwepo na mazingira Magumu ya Kufanya kazi kitu ambacho kimemchangia kutoandikisha matokeo mazuri, akimnyoshea Kidole cha Lawama mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu Hio kwa kukosa matumaini na yeye na Kuvuruga Mipango Ya timu hio.

Kufuatia Kipigo Hicho siku ya Jumatatu, MOFA Sasa wanashikilia Nafasi ya Tano kwenye msimamo wa Ligi ya NSL na alama Thelathini baada ya Mechi Kumi na Tisa, alama Kumi chini ya Viongozi wa Ligi Nairobi United wakiandikisha Ushindi kwa Mechi nane, sare Tisa huku wakipoteza Mechi tano.