RUDIGER NA ALABA WAPONA, VINI AKIPANGA KUBAKI REAL

Beki wa Ujerumani Antony Rudiger pamoja na David Alaba ni kati ya wachezaji wa Real Madrid ambao wanatarajiwa kurejea kikosini baada ya kumaliza kuuguza majeraha yao.

Wachezaji hao walikosekana katika mechi ya mchujo dhidi ya Manchster City hiyo jana na kumfanya kocha wa Real Don Carlo Ancelloti kumtumia beki mchanga Raul Asencio raia wa Uhispania.

Usiku wa kuamkia leo Madrid imeitandika Man City kichapo cha mabao 3-2 katika uwanja wa Etihad kwenye mechi ya klabu bingwa Ulaya.

Wakati hayo yakijiri Vinicius Jr ambaye usiku wa kuamkia leo kwenye mechi ya Uefa ameibuka mchezaji bora wa ngarambe hiyo hii leo amethibitisha kuwa kwa sasa yuko kwenye mazungumzo ya kurefusha mkataba wake na miamba hao wa Uhispania.

Vinicius ameeleza kuwa yuko tayari ya kuzidi kuichezea Real Madrid ambao ni mabingwa wa UEFA mara 15 kwa muda mrefu zaidi.