Jumla ya wanafunzi 25 katika kijiji cha Zobaki kule kaunti ya Tana River, wamekamatwa na viongozi wa idara ya usalama katika oparesheni ya kuwasaka watoto ambao, bado hawajende shuleni kufikia sasa.
Kulingana na Chifu wa eneo hilo Saidi Komora, ambaye pia aliongoza opareshini hiyo kwa ushirikiano na wazee mitaa katika eneo lake, watoto waliotiwa nguvuni ni wale waliokuwa wakiranda mitaani.
Komora amesema kuwa idara hiyo sasa, imeanzisha mikakati ya kuwasaka wazazi wa watoto hao, ili kuhakikisha kuwa wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, amesema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakitaja ukosefu wa karo kuwa mojawapo ya sababu kuu, ambazo huchangia suala la wao kukosa kuwapeleka wanao shuleni.

