Shirikisho la soka katika kaunti ya Kwale inalenga kuandaa mashindano yao ya kwanza ya soka la ufukweni mwaka 2025
Kulingana na taarifa ni kuwa kwa sasa usajili unaendelea kwa vilabu vya kaunti hiyo usajili ambao unatarajiwa kutamatika tarehe 25 mwezi huu.
Hili likiwa ni tukio la hivi punde baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Fkf kaunti ya Kwale mashindano ambayo mshindi anatarajiwa kushinda laki nne, nafasi ya Pili laki mbili na nafasi ya tatu na nne wakijishindia laki moja pesa taslimu za Kenya. Wakati hayo yakijiri;
Mohamed Mussa Omari mwenye umri wa Miaka Ishirini, hivi sasa ataichezea timu kubwa ya Bumbani stars Yenye makazi yake Huko kwale, hii ni baada ya kupandishwa Daraja Kutoka kwa timu ya Vijana.
Mohammed ambaye amekua akitumika kama Mshambuliaji nambari Moja kwa Muda sasa, amesaini mkataba wa Miaka miwili na miamba hao wanaoshiriki ligi Ya Divisheni ya pili.
Majukumu yake ya kwanza yatakua dhidi ya Busho Ocean star, siku ya Jumatano kwenye Michuano ya Kwale FKF cup.