ALIYEKUWA GAVANA WA KIAMBU FERDINAND WAITITU AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 12 GEREZANI AU FAUNI YA SHILINGI MILIONI 53.5.

Mahakama milimani inayo sikiliza kesi za Ufisadi nchini imemhukumu aliyekuwa gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, kifungo cha miaka 12 gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai kwa kutoa zabuni ya Shilingi milioni 588 kufanikisha ujenzi wa barabara mwaka wa 2018 kinyume cha sheria.

Waititu alipewa chaguo la kulipa faini ya shilingi milioni 53.5, kwa kosa hilo

Huku Mkewe Susan Wangari, akipatikana na hatia na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani au faini ya Shilingi laki 500,000.

Wakati huo huo, mahakama iliamua kwamba wafungwa wote wanatazuiliwa kushikilia ofisi ya umma kwa miaka 10.

Waititu alipatikana na hatia ya shtaka la kupokea Shilingi milioni 25,624,500 kutoka kwa kampuni – Testimony Enterprises Limited, mali ya washirika wa mkewe, kinyume na sheria za upeanaji wa zabuni nchini.

Pia amepatikana na makosa mengine matatu ya kuhusika na mali iliyoshukiwa kuwa kinyume cha sheria za ufisadi wa fedha za umma  kwani anadaiwa kutuma fedha kwa kampuni yake – Saika Two Estate Developers Limited kutoka Testimony Enterprises.

Kampuni yake ilipokea Shilingi milioni 12,410,500 kutoka Testimony Enterprises kati ya Julai 2, 2018, na Machi 13, 2019, na Shilingi milioni 6 kati ya Agosti 27 na Septemba 27, 2018.

Waititu pia alishtakiwa kwa kosa sawa na mkewe, baada ya kupokea kwa pamoja Shilingi milioni 7.2, kutoka kwa kampuni ya Testimony Enterprises.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *