KAKA WA DZUYA AUKATA MZIZI WA FITINA

Hisia mbalimbali kuhusu kuondoka kwa Feyswal Dzuya katika klabu yake mpya SS Assad zimezidi kuibuliwa mitandaoni mashabiki wakitoa maoni yao hadi sasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kaka na ajenti wa Dzuya, Ali Moha ni kuwa Dzuya hajaondoka kambini Kwale kwa sababu ya mshahara au marupurupu japo bado inaaminika kuwa kati ya mambo yaliyochangia.

Moha ameiweka wazi kuwa Dzuya amekuwa na tofauti zake na kocha Phelix Ogutu. Moha amekanusha madai yaliyotolewa na Ogutu wiki kuwa Dzuya aliona halipwi au hapati marupurupu ndiposa akaingia mitini.

Kwa sasa inaminika Dzuya amekuwa nyumbani Magarini eneo la Mjanaheri kwa muda akionekana katika uwanja wa Beach Bay akishuhudia mechi na hata mazoezi.