LIVERPOOL KUPUMZISHA WACHEZAJI

Kocha wa Liverpool Arne Slot anasema analenga kuwapumzisha wachezaji wengi wa kikosi cha Kwanza kesho katika mechi ya Carabao

Liverpool leo itakuwa inamenyana na Southampton kwenye mechi ya Carabao na Slot anasema wachezaji kama Diogo Jota na viungo kama Szoboslai na Alex Mac Allister huenda wakazidi kupumzishwa.

Hata hivyo sajili ya majira ya kiangazi Federico Chiesa Kulingana na Arne Slot huenda akapata dakika za kutosha tangia kuhusishwa mara ya mwisho mwezi September

Liverpool kwa sasa iko na muendelezo wa matokeo mazuri, ikiongoza kwenye mashindano ya Uefa na ligi kuu ya Uingereza tangia Arne Slot kuchukua timu hiyo kutoka kwa Jurgen Klopp