Wakaazi wa pwani ndani ya masaa 24 yaliyopita wamezidi kuutumia mtandao wa facebook na kupongeza tukio la klabu ya Manchster United kumsajili Emmanuel Ziro mwenye asili ya kikenya ambaye anaaminika mizizi yake iko katika kaunti hii ya Kilifi.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 15 alisajiliwa kwenye timu ya vijana wachanga ya Red Devils baada ya kufuatiliwa kwa muda na maskauti wa Uingereza.
Taarifa zasema kuwa kabla ya kusajiliwa na Manchster United alikuwa amelengwa na vilabu kadhaa ambavyo ni pamoja na Liverpool pamoja lakini pia Arsenal.
Ziro kupitia mtandao wake wa Instagram amewashakuru Man U kwa kuwa na imani naye na kumsajili, pia amewashukuru wanafamilia wake kwa kumpa sapoti ya kutosha.

